Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA leo June 30, 2017 pamoja na kutambua bei kikomo za bidhaa mbalimbali za Petrol, imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya Petrol ambazo zitaanza rasmi kutumika kuanzia July 1, 2017.
Hii ni mara ya kwanza kwa Mamlaka hiyo kutangaza bei elekezi za mafuta siku ambayo sio Jumatano ya kwanza ya mwanzo wa mwezi kwa kuwa hutangazwa kodi na Serikali.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Eng. Godwin Samwel amesema:>>>”Si kawaida bei za mafuta kutangazwa siku ambayo si Jumatano ya kwanza ya mwezi kama utaratibu ulivyo kwamba bei za mafuta huwa zinatangazwa Jumatano ya kwanza ya mwezi lakini mara nyingi July haiwi hivyo kutokana na kwamba Serikali huwa inakuwa imetangaza kodi mpya.
“Kwa hiyo, utekelezaji wa kodi unaanza tarehe Moja mwezi wa Saba kila mwaka. Sisi kama Wadhibiti ambao tunadhibiti huduma hii ya mafuta ni kwamba imebidi tutekeleze kwa kutangaza bei leo ili zianze kutumika kesho kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2017 ambayo kulikuwa na kipengele cha kuongezeka Shilingi 40 kwa kila lita.” – Eng. Godwin Samwel.
Wizara ya Mambo ya Ndani, IGP wamezungumza kuhusu mauaji ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji!