Katika zile zilizosikika kwenye 255 ya February 18, Story ya kwanza kusikika inawahusu wasanii Maua Sama na Grace Matata.
Grace Matata amesema alikutanishwa na meneja wa Maua na kumwambia wanaweza kufanya kazi nzuri wakiwa pamoja ingawa Maua yuko chuo lakini tayari wameshafanya kazi moja na wanatarajia kufanya video atakapofunga chuo mwezi huu huku kukiwa na mipango ya wawili hao kuendelea kufanya kazi nyingi zaidi.
Msanii Stara Thomas ameachia single mpya ambayo ni ya Kibongo Fleva tofauti na awali alipokuwa akifanya Gospel baada ya kuokoka, Stara amesema kuwa alikuwa anafanya Gospel kwa sababu aliokoka lakini na hakuingia kwa sababu anataka pesa.
Stara amesema Gospel anaifanya kwa sababu ya kumtumikia Mungu, lakini anakuwa huru zaidi kwenye Bongo Fleva kwa sababu ana uwezo wa kufanya kama biashara tofauti na muziki wa Gospel.
Story ya tatu kusikika inahusu msanii Mabeste ambaye amesema kuwa tofauti na muziki ameamua kuingia kwenye biashara na tayari amefungua kampuni ya kuprint t-shirt ambayo itamsaidia kuongeza kipato kwa sasa.
Mabeste amesema kuwa atakuwa anaprint t-shirt za wasanii na watu mbalimbali ambao watahitaji huduma hiyo.
Bonyeza play kusikiliza story yote.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook