Zilizosikika kwenye 255 leo ipo inayomhusu Fredrick Bundala ambae amekuja na kitabu kinachozungumzia maisha ya Mtemi Mirambo wa Tabora, amesema kitabu hicho ni idea iliyozoeleka nchi za nje na baada ya kupitia mitandao akagundua Audio box kwenye soko ni kitu kikubwa sana na anapenda sana kusimulia matukio kama alivyowahi kufanya katika documentary kuhusu Mv Bukoba.
Aliona ana uwezo wa kutengeneza kitabu hicho, hivyo akatengeneza kitabu katika mfumo wa sauti (Audio Box) ambapo mtu atapata story yote kwa kusikiliza sauti inayosimuliwa.
Baadhi ya wasanii wameonekana kuhamia kwenye jukwaa la siasa, Mr. II (Sugu), Prof. Jay, Afande Sele na wengine wametangaza pia kuingia huko.. Juma Nature amesema alipanga kufanya hivyo na watu walimfuata, kwa mwaka huu ameona asigombee, kama angegombea Ubunge Temeke anaamini angepita.
Juma amesema akipata nafasi ya kuwa Mbunge jambo la kwanza kufanya kwa wananchi wake ni kushughulikia barabara ya Mbagala, Hospitali pamoja na Soko.
Msanii huyo amesema atagombea Ubunge kupitia chama chochote atakachoona kina msingi mzuri.
Wasanii wa Bongo Fleva nao ni wajasiriamali.. Jokate, AY, Daimond Platnumz wapo kwenye list ya wengi ambao wanafanya muziki lakini nguvu yao wanaiweka kwenye biashara pia.
Ruby ni moja ya wasanii wa kike ambao wanafanya poa kwa sasa kwenye muziki, Ruby amesema anapenda kuwa designer na anatarajia kuja na kitu kinachoitwa ‘Kilemba cha Ruby’ ambayo inahusiana na mambo ya fashion.
Idea ya Ruby anasema imekuja kutokana na kupenda kudesign vilemba tangu akiwa mdogo.
Isikilize hapa 255, bonyeza play mtu wangu..
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook