Ile kesi iliyokuwa imefunguliwa na mganga aliyedai kuwa anamdai msanii AT imemalizika rasmi jana baada ya kukata rufaa, akipiga story kwenye 255, AT amesema kesi hiyo imemalizika rasmi jana baada ya mganga huyo kukata rufaa lakini alikosa ushahidi na baadae iligundulika kuwa hakuwa na sifa za kuwa mganga kwa kuwa alikuwa hajasajiliwa kufanya kazi za uganga.
Weekend hii msanii Izzo Bizness atafanya show mkoani Mbeya ambayo imepewa jina la ‘Home Sweet Home Easter Season Concert‘, Izzo amesema show hiyo itafanyika tarehe 05 April, safari hii itakuwa tofauti kwa kuwa anategemea kuambatana na producer Duppy kwa ajili ya kufanya usaili na mtu atakaeshinda atafanyanae kazi, pamoja na surpise nyingi ikiwemo kuonyesha live video ya wimbo wake wa ‘Kidawa’ kwa mara ya kwanza.
Leo wasanii mbalimbali pamoja na wadau wa muziki wamekutana mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge aliyefariki Jumamaosi iliyopita, akiongea kwenye 255 Kwembe ambae ni mdogo wake marehemu ambae amesema taratibu za kuupumzisha mwili wa marehemu zinaendelea katika makaburi ya familia huko Mkuyuni.
#RIP #AbdulBONGE
Kusikiliza story zote kweny 255 bonyeza play hapa chini…
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook