Jana staa wa Bongo, mrembo Wema Sepetu alifanya party ya Birthday yake ambapo alialika watu wengi kufurahi naye kwenye sherehe hiyo… mbali ya kujizawadia gari kali kabisa aina ya Range Rover, Wema alizindua pia brand ya lipstick zake.
Meneja wa Wema ambaye ni Martin Kadinda amesema biashara ya lipstick ilikuwa mpango wao wa siku nyingi lakini Wema aliikatia tamaa.. Martin amesema aliweka nguvu nyingi kuhakikisha biashara hiyo inafanikiwa na imezinduliwa rasmi jana.
Hongera kwa MwanaBongo Fleva Omary Faraji Nyembo aka Ommy Dimpoz, kwa ushindi wa Tuzo nyingine toka Marekani.
Meneja wa Ommy ambaye anaitwa Mubenga amesema wanashukuru sana kwa support ya Kura walizopigiwa mpaka kuibuka na ushindi huo, kingine wanajipanga sasahivi baada ya kutua Bongo itakuwa mwendo wa nyimbo kali pamoja video.
Moja ya mastaa ambao wamekua wakiwa na headlines za muziki TZ ni Mr. Blue ‘Bayser’, kuna wakati alitamani kuacha muziki? Jibu lake ni YES !! Blue anasema kuna wakati alijikuta njia panda ya nini afanye baada ya mama yake mzazi kufariki.
Mr. Blue amesema hakuwahi kuishi na mtu mwingine zaidi ya mama yake mzazi, hivyo hakujua baada ya msiba wa mama yake anaanza vipi maisha… baada ya kuachia hits kadhaa ikiwemo ‘Pesa‘ alirudi vizuri na kuamua kuendelea na muziki mpaka sasahivi.
Mr. Blue, Ommy Dimpoz na Martin Kadinda sauti zao utazisikia pia kwenye hii U Heard ya Soudy Brown iliyorekodiwa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE