Najua kila mmoja ambaye amekuwa akiisikiliza Bongo Fleva kwa kitambo hivi atakuwa ameshuhudia mastaa kibao wakivuka border na kupiga show nje ya TZ, kama Marekani na kwingineko.. kwani Muziki wa Bongo unasikilizwa maeneo ya huko?
Mmoja ya Mapromoter wakubwa ambao wamekuwa wakiwapeleka sana mastaa wa Bongo kupiga show Marekani amesema siku hizi imekuwa kawaida kusikilizwa muziki wa Bongo au Afrika kwenye Clubs za Marekani…
kingine amesema kuhusu story za wasanii wa TZ kupiga show sehemu ambazo zinakuwa na watu wachache, amesema watu wenye asili ya TZ au Afrika ni wachache kwa hiyo kama kukiwa na show sio rahisi kuandaa show ya msanii kutoka TZ au Afrika kwenye Ukumbi mkubwa wakati watu watakaoingia kucheki show ni wachache, kwa hiyo ni lazima ipatikane sehemu ambayo inaweza kukutanisha watu wachache.
Wapo mabingwa wa kuiga sauti za watu maarufu, kumbe sauti ni mali?! YES, majibu yametoka kwa Mwanasheria ambae amesema kuitumia sauti ya mtu anatakiwa mwenye sauti alipwe au kuwe kuna makubaliano maalum, ikiwa kinyume na hapo basi Sheria hairuhusu kutumia sauti ya mtu
Tour ya staa wa Muziki kutoka Uganda ndani ya TZ imezaa matunda mengine, staa huyo ni Jose Chameleone.. matunda yenyewe ni collabo ambayo tayari imeshafanyika kati yake na Barnaba..
Story imegusa kwenye 255 ambapo Barnaba amesema tayari kazi ya collabo yao imekamilika na itaachiwa muda wowote baada ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumapili October 25 2015.
Story zote hizi hapa, nimerekodi kipande cha #255 kwenye show ya XXL ya Clouds FM October 21 2015.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.