Jumamosi ya July 15 2017 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilicheza game yake ya kwanza ya kuwania kufuzu kucheza michuano ya CHAN 2018 dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda katika uwanja wa CCM Kirumba, Taifa Stars iliambulia sare ya 1-1- dhidi ya Rwanda goli lao likifungwa na Himid Mao kwa penati na Rwanda lilifungwa na Dominique.
Baada ya mchezo huo uliyochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba, kocha wa Taifa Stars Salum Mayanga na nahodha wa Taifa Stars Himid Mao waliongea na waandishi wa habari kuhusiana na mchezo huo wanadhani walikwama wapi?
“Tumepata sare ya 1-1 nyumbani hayo sio matokeo mazuri kwetu lakini tayari tumepata sare ni jukumu langu mimi na wenzangu kuangalia mapungufu yaliojitokeza katika mchezo huu tuyafanyie marekebisho ili tukafanye vizuri mchezo wa marudiano” >>> Salum Mayanga
VIDEO: Taifa Stars ilivyoambulia sare ya 1-1 vs Rwanda CCM Kirumba