Usiku wa September 20 2017 club ya Real Madrid ilirudi katika uwanja wake wa Santiago Bernabeu kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu Hispania dhidi ya Real Betis, Madrid walirudi wakiwa na staa wao Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa amefungiwa game nne na LaLiga.
Real Betis wamefanikiwa kuondoka na point tatu Santiago Bernabeu baada ya kuifunga Real Madrid kwa goli 1-0, goli la Real Betis likifungwa dakika ya 90 na Sanabria Ayala, kipigo hicho kinavunja rekodi mbili za Real Madrid ambapo game hiyo ndio inakuwa ya kwanza kumalizika kwa Real Madrid kutofunga goli toka April 2016 dhidi ya ManCity (0-0).
Real Madrid pia wanashindwa kuendeleza rekodi yao ya kupata ushindi katika michezo 73 mfululizo, rekodi ambayo ilidumu kwa miaka baada ya kuwekwa na club ya Santos mwaka 1963, Real Madrid wameifikia rekodi hiyo ya Santos lakini wameshindwa kuivunja.
Matokeo ya game za LaLiga zilizochezwa usiku wa September 20 2017 #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/FxpZDSHgec
— AyoTV (@AyoTV) September 20, 2017
Matokeo ya game zote tano za EFL Cup zilizochezwa usiku wa September 20 2017 #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/QkWKoYuqJu
— AyoTV (@AyoTV) September 20, 2017
ALL GOALS: Simba vs Mwadui FC September 17 2017, Full Time 3-0