Kama ni shabiki wa soka la bongo najua ukiachana na usajili wa Haruna Niyonzima kutoka Yanga kwenda Simba na Ibrahim Ajibu kutoka Simba kwenda Yanga, usajili mwingine uliyochukua headlines katika soka la Bongo ni usajili wa nahodha wa zamani wa Azam FC John Bocco kutoka Azam FC kwenda Simba.
Uhamisho wa Bocco ni uhamisho ambao watu wengi hawakuutegemea kutokana na John Bocco ameichezea Azam FC kwa muda mrefu, hivyo wengi walikuwa wanahisi labda Bocco anaweza akastaafu soka akiwa Azam FC, AyoTV imempata katika exclusive interview Himid Mao wa Azam FC ambaye amecheza na Bocco kwa muda mrefu, alipokeaje taarifa za John Bocco kuondoka? kwa nini wengi wamehama Azam?
“Tangu naingia Azam John Bocco ndio alikuwa room mate wangu hadi anaondoka Azam hivi juzi, kabla ya hapo alikuwa Philipo Alando ambaye ni team meneja kwa sasa, taarifa za John Bocco kuondoka Azam nilizipokea kwa mshituko lakini mchezaji mpira hana sehemu permanent sehemu yako permanent ni uwanjani ndio unatakiwa uipiganie”
“Wakati Bocco anaondoka Azam mimi nilikuwa camp timu ya taifa yeye hakuwepo alikuwa anaumwa hata mechi ya mwisho ya Azam FC ya msimu hakucheza, kwa hiyo hata wakati anaodoka alinipigia tu simu akanipa taarifa kuwa anaenda timu nyingine na mimi nikamtakia kila la kheri”
VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0