Michezo

Timu iliyomsajili Emmanuel Okwi kwa kipindi cha miezi mitatu

on

Baada ya mshambuliaji wa zamani wa Simba na timu ya taifa ya Uganda Emmanuel Okwi kuvunja mkataba na timu yake ya Sønderjyske ya Denmark, leo February 1 2017 zimeripotiwa taarifa za timu aliyojiunga nayo.

Okwi amejiunga na klabu yake ya zamani ya Sports Club Villa ya kwao Uganda kwa ajili ya kumalizia msimu, ina maana atakuwa na timu hiyo katika kipindi cha miezi mitatu.

Maamuzi ya Okwi kujiunga na timu ya Sport Club Villa kwa kipindi cha miezi mitatu yanatafsirika kama kucheza kujiweka fiti kwa ajili ya maandalizi ya kurejea Simba wakati wa usajili, kama utakuwa unakumbuka Okwi alijiunga na Sønderjyske  ya Denmark na aliamua kuvunja mkataba baada ya kuona hana nafasi.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments