Baada ya wekundu wa Msimbazi Simba SC kutwaa Ubingwa wa tatu wa Ngao ya Hisani kwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penati 5-4 uwanja wa Taifa Dar es Salaam, headlines zilikuwa ni Ngao ya Hisani waliyopewa Simba baada ya game.
Ngao ya Hisani waliyopewa Simba ilikuwa ina makosa ya kiuandishi, kitendo ambacho kilifanya iwe stori kubwa na kuzungumzwa katika mitandao mbalimbali kiasi hata cha tovuti ya BBC Africa kuandika habari hiyo.
Baada ya game Ngao iliyotolewa iliandikwa ‘Community Sheildx‘ badala ya kuandika ‘Community Shield’ kama inavyotakiwa, waandaaji wa Ngao hiyo ambao ni shirikisho la soka Tanzania TFF wameomba radhi kwa kosa hilo.
VIDEO: Penati ilizoipa Simba Ubingwa wa Ngao ya Hisani vs Yanga