Habari za Mastaa

“Nilipanic nilichokiandika Insta kuhusu Zari” – Diamond

on

Leo June 21, 2017 kupitia XXL ya Clouds FM Mwimbaji staa wa Bongofleva Diamond amezungumzia kwa mara ya kwanza tangu kupost picha na ujumbe kwenye Instagram yake juu mama watoto wake ‘Zari’ kufuatia picha aliyopiga akiwa na mwanaume akiogelea.

Diamond amesema baada ya kuiona picha hiyo alipanic na kuandika ujumbe ule ambao baada ya kusambaa alifuatwa na Zari na alipomuelewesha alimuelewa huku baadhi ya mastaa wa Afrika wakiwepo P Square na Fally Ipupa wakimpigia simu kumpoza hasira.

>>>“Mara ya kwanza nilipoona picha ya Zari kapiga na mtu kwenye maji nilipanic na nilichokiandika kwenye insta yangu nilimaanisha. Baada ya post yangu ya insta wasanii wengi walinipigia simu. P Square na Fally Ipupa walinicheki. Zari baada ya kuona post yangu Insta alikuwa ofisini, alirudi nyumbani na aliponielewesha nilikuwa mpole.” – Diamond Platnumz.

ULIPITWA: Majibizano ya Diamond Platnumz na Zari 

Soma na hizi

Tupia Comments