Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA leo limetoa maamuzi kuhusiana na mvutano uliopo kati ya Cardiff City dhidi ya club ya Nantes FC ya Ufaransa kuhusiana dau la usajili la marehemu Emiliano Sala.
FIFA imewaagiza Cardiff City kulipa pound milioni 5.3 kwenda Nantes kama ada ya uhamisho wa Emiliano Sala aliyefariki siku chache baada ya kusaini Cardiff akitokea Nates ila akapata ajali na kupoteza maisha akiwa katika ndege ndogo binafsi January 21 2019.
Baada ya ajali hiyo Cardiff walikataa kumalizia pesa za malipo ya usajili wa Sala aliyesajiliwa kwa pound milioni 15 wakidai kuwa mkataba umevunjika kwa sababu mchezaji huyo kafariki.
EXCLUSIVE: SAMATTA KAFUNGUKA DILI LAKE KWENDA ENGLAND, VIPI CHAMPIONS LEAGUE