Msanii na video vixen maarufu Bongo Giggy Money amezichukua headlines tena kufuatia post yake aliyoamua kupost mtandaoni akiwa pamoja na mzazi mwenzake ambaye ni mtangazaji wa Choice FM MO J.
Giggy kupitia ukurasa wake wa instagram ameacha maswali kwa watu baada ya kupost picha akiwa na MO J na kuandika mzazi mwenzangu, post hiyo inakuja ikiwa ni wiki kadhaa zimepita toka Giggy akanushe kuwa Myra sio mtoto wa MO J.
Sasa leo watu wanajiuliza mtoto wa Giggy Money anayejulikana kwa jina la Myra baba yake ni nani MO J au Stan? AyoTV na millaradyo.com zitamtafuta Giggy Money azungumzie taarifa hizi na kama amerudiana tena na MO J.
GIGY MONEY: “Mo J alitoka na House Girl, Mimi nikawa natoa pesa ya matumizi”