Michezo

Ushindi wa Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar umeirudisha kileleni (+Pichaz)

on

Baada ya malalamiko ya muda mrefu kuhusu klabu ya Dar es Salaam Young Africans kuwa na viporo vingi, hatimae April 16 2016 wamemaliza michezo yao ya viporo kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Yanga walikuwa na michezo ya viporo mitatu na watani zao wa jadi Simba walikuwa wakilalamika Yanga kupendelewa kwa mechi zake kusogezwa mbele mara kwa mara, hivyo hawakuwa radhi kuendelea kucheza wakati wakihisi kuna dalili za upangaji wa matokeo.

DSC_0303

Mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar hakuwa mwepesi kwa Yanga kwani Mtibwa walionekana kuwa na kikosi kizuri, kitu ambacho kilipelekea dakika 45 za kwanza kumalizika kwa kutofungana, mambo yalibadilika dakika 2 baada ya mchezo kuanza kipindi cha pili pale winga mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva alipoipatia Yanga goli la kuongoza na hatimae mchezo kumalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

ase

Msimamo wa Ligi Kuu Ulivyo kwa sasa

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

KAMA ULIIKOSA VIDEO YA MAGOLI YA MECHI YA YANGA VS MWADUI FC, FULL TIME 2-1

Soma na hizi

Tupia Comments