Mix

Picha 15: Mvua ya Dar zilivyompeleka RC Makonda Jangwani leo

on

Dar es salaam imekuwa moja ya majiji yanayosumbuliwa na kero za mafuriko haswa katika kipindi cha mvua, ni siku kadhaatu baadhi ya watu walilazimika kuhamishwa katika maeneo yao ya makazi kwa kukwepa miundombinu mibovu.

Leo April 16 2016 mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alilazimika kufunga safari kuelekea katika baadhi ya maeneo kujionea hali ilivyo baada ya mvua kuharibu miundombinu 

Kama mnavyoona,leo tumepita katika baadhi ya maeneo ikiwa ni pamoja na hapa Jangwani na kukuta hali si shwari, mitaro hii imeziba eidha kwa uchafu baada ya watu kutupa taka katika mitaro, lakini jambo la pili ni watu kujenga kwenye mikondo ya maji ’ ;-Paul Makonda

‘Kuna maeneo yamejengwa bila kuzingatia namna ya kupitisha maji, jambo ambalo linasababisha pia kuwa na ukwamishaji wa maji.’ ;-Paul Makonda

Ningewaomba wananchi kujiadhari kukaa kwenye mazingira hatarishi, pia kwa serikali ni kuhakikisha watu wanaotoa vibali kuangalia kutoa vibali katika maeneo yenye vikondo ya maji

‘Natoa pole kwa watu ambao maji yameingia majumbani kwao, lakini pia tusiendelee kukaa katika mazingira hatarishi na tuangalie maeneo ambayo ni salama kwetu’ ;-Paul Makonda

AW1A1537

Mkuu wa mkoa Paul Makonda akionyeshwa maji yalivyosambaa

AW1A1539

AW1A1550

AW1A1551

Wananchi wakizungumza na mkuu wa mkoa Paul Makonda

AW1A1561

AW1A1564

AW1A1569

AW1A1579

AW1A1582

AW1A1590

AW1A1595

AW1A1597

AW1A1604

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments