Hii ni stori nyingine tena ya 2014 ambayo inaingia kwenye list ya zile stori ambazo ukishaisoma au kuipata unaanza kufikiria mara mbilimbili na kujaribu pia kutengeneza picha yako mwenyewe kama upo eneo la tukio.
Watu wa karibu wa Mtuhumiwa huyu walijitokeza Mahakamani ili kuangalia kama ndugu yao aitwae Simon Ngozi (21) ataweza kupata dhamana kwenye kesi inayomkabili ya kubaka mtoto wa miaka tisa.
Imetokea Kenya ambapo jamaa alikua amepelekwa Mahakamani Makadara Nairobi lakini ghafla akamshangaza kila mtu baada ya kutaka kumaka Mwanamke aliekua karibu yake baada ya kuanza kumshikashika.
Mshukiwa huyu alikuwa kortini kujibu tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka tisa April 2014 ambapo wakati anataka kumbaka Mwanamke huyu Mahakamani tena kwenye eneo la wazi, alimpiga mtama kwanza Mwanamke huyo lakini kwenye purukushani zake hakufanikiwa manake Polisi walimuwahi.
Shughuli za Mahakama zilisimama kwa muda baada ya tukio hilo kutokea ambapo baada ya hapo Mwanamke alietaka kubakwa alisema ‘nilikua nimeketi karibu naye na mara ya kwanza alilishika begi langu nikalisogeza mbali nikidhani ni mwizi lakini bila aibu akanishikashika tumboni kabla ya kunisukuma nikaanguka sakafuni
Baada ya hapo dada wa mtuhumiwa alimuomba mwanamke huyo kumsamehe ndugu yake akisema yuko katika hali hiyo baada ya mchumba wake kumtoroka kwa sababu ya kesi ya ubakaji.
Hili linakua tukio jingine mimi kulisikia mwaka 2014 la kituko Mahakamani baada ya mawili ya Mwanza ambapo moja ni Mahabusu kujipaka kinyesi na kujaribu kutoroka akidhani hiyo mbinu itasaidia mtu asimshike, mwingine ni alievua nguo zote kushinikiza atendewe haki kwa kisa cha mauji alichobambikiwa.
Kituko kingine ambacho kilivunja rekodi kabisa ni cha Wafanyakazi wawili wa Mahakama nchini Italia kufanya Hakimu kuahirisha kesi baada ya wawili hao kuonekana wakifanya mapenzi kwenye chumba cha pili pembeni ya chumba kilichokua kinaendeshewa kesi.
Ungana na mimi mitandaoni kwa kubonyeza hapa ili niwe nakutumia kila kinachonifikia >>> Twitter Instagram facebook zikiwemo pichaz, videoz na taarifa mbalimbali.