Miongoni mwa stori za town nilizozipata ni hii ya Mamba kuuwawa Block 41 Kinondoni Dar es salaam kwenye area ambayo wanaishi watu kadhaa maarufu wa Tanzania akiwemo Kalapina wa kikosi cha Mizinga, hii ni nyuma ya bestbite Mamba huyu akiwa ametokea kwenye bwawa nyuma ya 41 Records.
Bwawa limezungukwa na nyumba kwenye eneo la kwa Kisamo zamani Kajima ambapo kwenye hili bwawa zamani kidogo kulikua na Mamba wawili ila baada ya kugundulika mmoja akachukuliwa na watu wa Wanyama ila mwingine hakuonekana.
Tukio la jana ilikua saa nane usiku ambapo mamba huyu alijitokeza barabarani mtaani ndipo majirani wakamuita mtu pekee mwenye bunduki kwenye huo mtaa ili amuue kwa sababu mwanzoni kabla hawajajua walikua wanahofia kumuua wakidhani ni kosa la kisheria.
Baada ya kuuwawa Defender ya Polisi ikamchukua huyu anaeitwa Mamba baadae alfajiri ambapo unaambiwa kwenye picha hapa anaonekana mdogo ila ni Mamba mkubwa kabisa, siku ya mvua aliwahi kutoka nje ya Bwawa tena ambalo alitisha sana watu ila muda mfupi baadae akarudi ndani ya Bwawa.
Ripota wa nguvu Ramaman kutoka Block 41 amenitumia hizi picha na kusema walifanikiwa kumuua huyu Mamba baada ya kumpiga risasi nne.
Unataka niwe nakutumia stori kama hizi na nyingine zote zinazonifikia kila wakati? jiunge na mimi kwenye twitter instagram na facebook kwa jina hilohilo la @millardayo ili niwe uzipate time hiyohiyo iwe usiku au mchana.