Ni taarifa ambazo zimetokea nchini Brazil ambako kombe la dunia linaendelea huku timu za Afrika zikiwa kwenye headlines ikiwemo Ghana ambayo imepigwa 2-1 na Portugal June 26 2014.
Taarifa ikufikie kwamba wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya Ghana Sulley Muntari na Kevin Prince Boateng wamefukuzwa mara moja katika timu hiyo kwa ukosefu wa nidhamu ambapo hizi stori zimethibitishwa na mtandao wa shirikisho la soka Ghana.
Boateng anayechezea Schalke 04 amefukuzwa kwa kutoa matamshi machafu kwa mkufunzi wa timu hiyo Kwesi Appiah wakati timu hiyo ilipokuwa katika mazoezi katika eneo la Maceio ambapo kwa upande wa staa wa soka anaeichezea AC Milan Sulley Muntari, ameadhibiwa kwa kumshambulia afisa mmoja wa kamati kuu ya timu hiyo.
BBC wameripoti kwamba Boateng amedaiwa kutojali matamshi aliyoyatoa zikiwa ni habari mbaya zilizotokea baada ya siku moja tangu serikali ya Ghana kutuma dola millioni 3 nchini Brazil ili kuwalipa wachezaji wa timu hiyo fedha zao za kushiriki michuano ya kombe la dunia kwa sababu kabla ya hapo walitishia kugomeamechi na Ureno kama wasingekua wamelipwa.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB