Mix

VideoFUPI: Shilingi milioni 335 zimesahaulika uwanja wa ndege Nigeria

on

Kutokea nchini Nigeria nimeipata hii ya taarifa ya Maafisa wa Serikali nchini humo jana wamefanikiwa kugundua magunia matano yaliyokuwa yamehifadhi burungutu za fedha kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kaduna.

Pesa hizo kiasi cha Naira milioni 49 ambazo ni zaidi ya shilingi za Tanzania milioni 335 zimepatikana kwenye eneo la kuhudumia wasafiri wanaoingia uwanjani hapo, ziligunduliwa wakati wa ukaguzi wa kawaida wa mizigo uwanja wa ndege.

Msemaji wa Tume ya Uhalifu wa Kifedha nchini humo, Wilson Uwujaren amesema magunia hayo yalikuwa na burungutu 200 za noti mpya, ambazo zilikuwa bado hazijafunguliwa kutoka kiwandani, amesema uchunguzi unaendelea kubaini nani mwenye magunia hayo.

VIDEO: ‘Mimi sio Mwanasiasa ninayetafuta sifa za kijinga’ – Paul Makonda, Tazama hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments