Mwanamume mmoja Raia wa Nigeria imebidi alazwe kwenye hospitali ya taifa ya Kenyatta Nairobi Kenya baada ya kugundulika alikua na mzigo wa dawa za kulevya wa vidonge 57 tumboni mwake.
Huyu jamaa alikua anazisafirisha hizi dawa kutoka Lagos kwenda Bangkok lakini ghafla akaanza kupata maumivu baada ya kuchelewa kufikisha mzigo aloubeba tumboni mwake baada ya ndege waliyokua wakisafiria kutua Nairobi kwa dharura.
Ilitua kwa dharura baada ya rubani kuumwa ghafla hivyo kulazimu ndege kutua Nairobi kisha abiria wote kupelekwa hotelini na hapo ndio Mnigeria huyu akaanza kuhisi maumivu makali tumboni.
Simon Ithae ambae ni mkuu wa mawasiliano hospitali ya Kenyatta amesema ‘alitueleza amemeza vidonge na alikua akiamini ndicho chanzo cha maumivu hivyo alipoona hawezi kustahamili aliita Polisi akidai ameumizwa na anahitaji kupelekwa hospitali lakini lengo lake ni apange njama na madaktari kutoa dawa za kulevya bila yeye kukamatwa na aendelee nazo na safari lakini mipango yake haikufanikiwa kwa sababu Madaktari walimpa chakula ili kutoa dawa hizo na kisha wakawapa taarifa Polisi.
STORI: Julius Kepkoech – TZA Kenya.