Sio kitu kigeni kuona watu wenye umri zaidi ya miaka 18 wanakunywa Pombe wanalewa na hata pombe hiyo kugharimu maisha yao ila sio kawaida kukutana ama kuona mtoto wa miaka kati ya 14-17 ni mlevi wa kupindukia na mtumiaji pia wa dawa za kulevya.
Ripoti mpya iliyotolewa na Mamlaka ya kudhibiti vileo nchini Kenya (NACADA) inaonyesha kwamba ni watoto zaidi ya MILIONI MOJA nchini humo wenye umri kati ya miaka 14-17 ambao ni watumiaji wakubwa wa pombe na dawa za kulevya.
Ripota wa millardayo.com na AyoTV Kenya Julius Kepkoech amesema mwenyekiti wa NACADA John Mututho ameisema hii wakati alipowatembelea Wanafunzi 16 waliokamatwa wakiwa wamelewa mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo sasa wamefikishwa kwenye Mahakama ya Baricho.
Hakimu mkuu wa Baricho Hezekiah Keago ameamuru Wanafunzi hao baadhi kurudishwa mikononi mwa wazazi ili kufanyiwa ushauri nasaha lakini pia vilevile Wanafunzi wengine waliobakia kati ya hao wamehukumiwa kwenda jela ya Watoto Muranga.
Ushahidi uliotolewa Mahakamani umeonyesha kwamba hawa Wanafunzi ambao wamekamatwa kwa ishu ya pombe, walihusika kuinywa pia pombe iliyopigwa marufuku nchini Kenya ambayo ina kemikali hatari kwa afya na iliua zaidi ya watu mia moja.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote iwe usiku au mchana iwapo utakua umejiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> twitter Insta FB