Kupitia Uheard leo July 20, 2017 imemfikia hii mtangazaji Soudy Brown kuhusu Young Dee na Amber Lulu ambao walidaiwa kuwa mapenzini lakini taarifa nyingine zikasambaa kuwa waili hao wamegombana.
Soudy amewatafuta Young Dee na Amber Lulu na kupiga nao story huku ikidaiwa kuwa Amber Lulu amefuta tattoo ya taswira ya Young Dee aliyokuwa amechora.
>>>”Hamna mwanangu tu, Mnyamwezi wangu. Nimechora tattoo mpya ile ilikuwa imechoka sana ndio nikabadilisha. Sifichi, hatujazinguana chochote sisi ni washikaji siku zote. Young Dee hajawahi kuwa mpenzi wangu, ni washikaji tu. Kwani Soudy ulishawahi kumuuliza Young Dee kama mimi ni mpenzi wake? Mimi mbona nina Bwana wangu, Young Dee ni msanii mwenzangu tu.” – Amber Lulu.
Naye Young Dee alikuwa na haya alipoulizwa kuhusu kuwa mapenzini na Amber Lulu.
“Tumeachana na nani? Nimekuambia am single…sijawahi kuishi na Amber Lulu, hakuwahi kuwa mwanamke wangu. Mimi sijui maana alichora mwenyewe kwa kupenda na kama kafuta kafuta kwa kupenda mwenyewe.
“Hakuna mtu aliyemwambia, sasa itanishtua kitu gani? Mimi naona kawaida siyo breaking news labla taarifa iliyonishtua ni hii ya Msiba wa Mama Zari lakini unaniambia taarifa ya kushtua ni hiyo ya kufuta tattoo! Hebu niache nifanye kazi.” – Young Dee.
Bonyeza Play hapa chini kuwasikiliza Young Dee na Amber Lulu…
ULIPITWA? Profesa J alivyorudi Mikumi kufanya sherehe ya pili ya harusi yake