Headlines za soka la Bongo December 17 zilikuwa ni stori za kiungo wa kimataifa wa Rwanda anayechezea klabu ya Dar Es Salaam Young African Haruna Niyonzima, kuwa klabu ya Yanga kupitia kwa katibu mkuu wake , ambaye ndiye mtendaji mkuu wa Klabu DK Jonas Tiboroha imeamua kumfungia kiungo huyo kwa muda usiowekwa wazi.
Amplifaya ya Clouds FM ilimtafuta katibu mkuu wa Yanga ambaye alithibitisha kuwa taarifa hizo ni za kweli ila taarifa rasmi ya klabu itatoka Ijumaa ya December 18 katika mkutano na waandishi wa habari, Niyonzima anatajwa kupewa adhabu hiyo kutokana na utovu wa nidhamu, ikiwemo kukiuka maagizo ya katibu kuwa ili ajiunge timu ya taifa ya Rwanda ni lazima barua ifike Yanga, kitu ambacho akikutimizwa na Niyonzima kwenda timu ya taifa moja kwa moja.
“Kuhusu stori za Niyonzima kusimamishwa hilo lina ukweli lakini kwa sasa hivi nisingependa kuliongelea sana hadi kesho mchana, siwezi kumjibia chochote Haruna kwani bado hajaongea na uongozi” >>>> DK Tiboroha
Unaweza sikiliza sekunde 40 za katibu wa Yanga kuhusu Niyonzima
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.