Mwimbaji Shilole alikuwa miongoni mwa mastaa waliopata nafasi ya kuzungumza usiku wa March 30,2019 kwenye harambee ya uchangiaji fedha kwa jailli ya kujenga bweni la wasichana katika shule ya wilayani Kisarawe ambapo shughuli hiyo iliandaliwa na DC Jokate Mwegelo.
Shilole alizungumza vitu vingi ambapo baadae kwenye miandao ya kijamii maneno yale yalionekana kama kulenga mzee wa Liquid Pierre na ndipo hapo watu walipoanza kufukua makaburi na kumbusha ya kale na mpaka alipo sasa.Hivyo Shilole kupitia ukurasa wake ameomba radhi kutokana na maneno yale aliyozungumza ikiwemo kumuomba radhi Pierre.
“Kwa Watanzania wenzangu,Kwanza, nikiri kwamba nimeona wengi niliowakwaza kutokana na maneno niliyoongea jana kwenye tukio liliondaliwa na rafiki yetu @jokatemwegelo(#TokomezaZiroKisarawe). Kwa kuwakwaza huko bila hata kwenda mbali kutoa maelezo yoyote, NAOMBA RADHI, MNISAMEHE SANA”
“Pili, nahisi kuna namna sijaeleweka au mimi sikuweka vizuri maelezo yangu. Ninyi mnanijua vizuri, mwenzenu mimi mara nyingi sana nimeongea vitu hadharani kwa kukosea kutokana na udhaifu na uwezo wangu mdogo kwenye kujielezea (hilo mnalijua, kwamba mie mwenzenu kidogo shule sikwenda na wakati mwingine kichwa changu kinapata moto na hiyo sio sifa). Sasa naomba mniruhusu kueleza kwa ufupi nia yangu”
“Hoja yangu mimi ilikuwa “Kuna vitu vya msingi hamzungumzi ila vitu vya ajabu mnazungumza…..” ukisikiliza ile video utasikia mstari huo. Hicho ndio kitu nlichotaka kueleza, sio kumkashifu Pierre au mtu mwingine yeyote. Iwapo Pierre ni mmoja kati ya watu waliokwazika, namuomba sana anisamehe. Lakini tuwe wa kweli, watu wengi wamewahi kusema hili (kuna vitu vya msingi havitangazwi), ila tu mimi kwa akili yangu ndogo nilishindwa kusoma mazingira na muda nikalisema jana. Nirudie tena kusema SAMAHANI”
“Nimeona wengi wakirudi nyuma kutafuta matukio yangu, kutafuta nilitokea wapi hadi hapa nilipo. Niwahakikishie kwamba mimi nafahamu upendo mkubwa wa Watanzania kwangu kiasi kwamba walinibeba hata pale nilipokosea, walinivumilia katika ujinga wangu na bado wanaendelea kunivumilia, wananipenda licha ya ulewa wangu mdogo (Kingereza na mambo mengine ambayo yamegeuka utani dhidi yangu), na walinipa nafasi kujifunza, kujirekebisha na kukua hadi hapa nilipo”
“Narudia tena, Nimekosea kama nilivyowahi kukosea mara nyingi, NAOMBA RADHI TENA, lakini zaidi ya yote naomba mfahamu sikuwa na nia mbaya, nilikosea tu namna ya kusema na niseme wakati gani.Asanteni. #ChiiiiiiiiiiiiWatanzaniaMtabakiKuwaJuuuu”
Ulipitwa na Prof Jay, Diva, Dj Fetty na Wolper walivyosimama kumtetea Pierre mtandaoni? Bonyeza PLAY hapa chini.