Wakali kutokea kwenye game ya Hip Hop nchini Marekani Pusha T pamoja na Rappa Drake kutokea Canada wameonekana kuendeleza bifu lao ambalo liliwahi kutokea miaka kadhaa iliyopita hii ni baada ya kuonekana kutupiana madongo kupitia ngoma zao.
Bifu hilo linaonekana kuendelea kati yao baada ya Pusha T kutumia picha ya Drake kama cover ya wimbo wake wa “The story of Adidon” ambapo wawili hawa wamekuwa wakitupiana madongo kupitia nyimbo zao.
Drake kupitia instagram story yake alijibu kuhusiana na picha hiyo aliyoitumia Pusha T na kusema kuwa “Hii picha ni ya mwaka 2007, nilipokuwa naigiza katika project flani kuhusiana na vijana weusi wanaohangaika katika sanaa ya burudani”
Mwaka 2016 Pusha T alizidi kumuhoji Drake katika mistari ya ngoma yake na kusema kuwa “It’s too far gone when the realest ain’t real” akimaanisha “Ni mbali sana ulipoenda ambapo uhalisia sio wa ukweli” kwenye “HGTV Freestyle .
Baada ya Drake kupata ujumbe huo aliamua kumjibu Pusha T kuhusiana na tuhuma za kutumia dawa za kulevya na kusema kuwa “Ulitengeneza baadhi ya chops na sasa unahisi utaua ndege wawili kwa jiwe moja? >>>You made a couple chops and now you think you Chapo” on “Two Birds, One Stone”.
Wakazi awatolea povu wakongwe wa Bongo Fleva