AyoTV

Waziri Mwakyembe baada ya kukagua uwanja wa Taifa na Uhuru kwa AFCON U-17

on

Bado siku tano tuweze kushuhudia fainali za AFCON U-17 2019 zitakazofanyika Tanzania kwa siku 14 kuanzia April 14 2019 hadi April 28 2019, Tanzania akiwa nchi mwenyeji wa michuano hii baada ya 2017 michuano hiyo kufanyika nchini Gabon.

Kuelekea kuanza kwa michuano hiyo waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe ameongea na waandishi wa habari baada ya kukagua maandalizi ya viwanja vya Taifa na Uhuru, uwanja wa Taifa ndio utatumika kwa ajili ya mechi za mashindano na Uhuru utatumika kwa ajili ya mazoezi.

Tayari hadi kufikia jana timu za taifa  za vijana za Morocco na Cameroon zimewasili Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo, michuano hiyo kwa mwaka huu itashirikisha mataifa nane kama ilivyokuwa awali, Cameroon, Morocco, Uganda, Angola, Senegal, Guinea, Nigeria na Tanzania nchi mwenyeji.

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments