Michezo

Daniel Sturidge kucheza dhidi ya Chelsea.

on

Daniel-Sturridge.png

 

Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturidge huenda akarejea uwanjani katika mchezo wa nusu fainali ya michuno ya kombe la Capitol one wakati ambapo timu yake itakapokuwa ikicheza na timu yake ya zamani ya Chelsea .

Kocha wa Liverpool ambaye kama Sturidge aliwahi kufanya kazi na Chelsea Brendan Rodgers amethibitisha kuwa Sturdige amepona na huenda akaonekana uwanjani katika mchezo huo wa marudiano .

Sturidge ambaye msimu uliopita alifunga mabao 25 kwenye michuano yote amekuwa nje tangu kuanza kwa msimu , ikiwa imepita miezi mitano tangu alioichezea Liverpool mwishoni mwa msimu uliopita .

JS45185526

Sturdige amekuwa akisumbuliwa na majeraha tofauti tangu aliporudi toka Brazil baada ya kombe la dunia hali ambayo imefanya asicheze mechi yoyote kuanzia mwezi wa nane mwaka jana hadi leo hii .

Mwezi wa 12 mshambuliaji huyu alisafiri kwenda nchini Marekani ambako alikwenda kupata tiba zaidi kwenye jeraha lake la misuli ya paja na kocha wake Brendan Rogers ana matumaini kuwa timu yake itafaidika kwa kurejea kwa Sturidge .

Liverpool inakutana na Chelsea katika marudiano ya mchezo wa nusu fainali ya kombe la capitol one baada ya timu hizo mbili kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa huko Anfield.

Tupia Comments