Leo June 25,2018 inatimia miaka tisa tokea dunia ipate taarifa za kifo cha mfalme wa muziki wa Pop duniani Marehemu Michael Jackson ambaye alifahamika duniani kote kutokana na upekee aliokuwa nao katika uchezaji pamoja na nyimbo zake ambazo zilipendwa na watu wengi ulimwenguni.
Marehemu Michael Jackson alipendwa zaidi na watoto kutokana na upendo na ukaribu aliokuwa nao kwa watoto wote ambapo hakujali rangi (race) na enzi za uhai wake Michael Jackson aliwahi pia kutembelea Tanzania na kukutana na Rais wa awamu ya pili wa Tanzania mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
Marehemu Michael Jackson alifariki June 25,2009 akiwa nyumbani kwake Holmby Hills, Los Angeles nchini Marekani ambapo alikutwa chumbani kwake na mmoja wa madaktari wake Conrad Murray akiwa hapumui na kukimbizwa hospitali ya Ronald Reagan UCLA Medical Centre.
Marehemu Michael Jackson aliwahi kushinda tuzo ya Grammy Awards katika wimbo bora wa RnB mwaka 1984, Grammy Award wimbo bora wa mwaka 1986, MTV video music award 1995,Billboard Music Award for spotlight 1989 na nyingine nyingi.
Marehemu Michael Jackson alitamba na ngoma kali ikiwemo Thriller, Bill Jean, We are the World, The way you make me feel, Beat It, You Rock My World, Earth song, Dirty Diana na nyingine nyingi ambazo bado zinaheshimika duniani kote mpaka leo.
Uwoya kafunguka tusiyoyajua “Nimepiga picha na Mama Mkwe, Dogo Janja nimemzidi vingi”