Tarehe 31 March 2015 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ameitisha waandishi wa habari na kutangaza kuwa ameanzisha Kinondoni Talent Search ambayo itahusika kusaka vipaji vya watoto wenye vipaji kama; Kucheza, Kuimba, Kuchekesha na vinginevyo.
Akizungumza na waandishi wa leo alisema; “Kinondoni Talent Search ni mpango wenye lengo kuu la kuwatambua vijana waishio kwenye wilaya ya Kinondoni wenye vipaji vya kuimba, Kuchekesha ambao wengi wao wapo katika mazingira magumu ya kiuchumi jambo linalowafanya kushindwa kuonesha vipaji vyao mwisho ndoto zao kufifia… Lengo kuu la mpango huu ni kuwawezesha kupata njia za kutimiza ndoto zao kupitia uwezo wao”
Kinondoni Talent Search inalenga kwanza, kuwatengeneza nafasi za mafanikio vijana wenye vipaji, kuwapatia mafunzo na kuwaunganisha na wadau muhimu waliopo kwenye sekta zao. Lakini kubwa zaidi, kutoa hamasa kwa vijana wote wa Wilaya ya Kinondoni na Tanzania kwa ujumla juu ya umuhimu wa kuendeleza vipaji vyao, kuepuka mambo yanayoweza kuviua na kuharibu malengo yao ya baadae, mfano matumizi ya dawa ya kulevya, ngono zembe na vitendo vya uporaji. Bila kusahau kuwakumbusha vijana wote kuwa ukimiliki kipaji unakuwa ajira, ni kujua tu namna ya kukitumia ili kikufae na kukufikisha utakapo.. na ndio maana kauli mbiu ya mpango huu ni ‘kipaji chako, ajira yako“– alisema DC Makonda.
Ili kuhakikisha mradi huo unafanikiwa kwa kiwango cha juu na kufikia lengo, Paul Makonda ametengeneza kamati maalum yenye wajumbe kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya pamoja na baadhi ya wasanii ambao wana uzoefu zaidi;
1. Jumanne Mrimmy – Afisa utamaduni (Manispaa ya Kinondoni)
2. Sebastian Mhowera – Afisa Uhusiano – (Manispaa ya Kinondoni)
3. Peter Msechu – Msanii wa Bongo Fleva
4. Jokate Mwegelo – Mwimbaji/Mbunifu
5. Mc-Pilipili -Mchekeshaji
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook