Kwenye U Heard ya jana ilisikika story ya vijana waliokuwa wanasoma Chuo cha Filamu cha TFTC Ubungo, kinachomilikiwa na muigizaji Pastor Myamba kulalamikia suala la chuo hicho kutowakabidhi vyeti baada ya kumaliza masomo.
Wanafunzia hao wamesema walisoma katika Chuo hicho kozi ya miezi sita mwaka 2013, lakini mpaka leo hawajapewa vyeti wala kucheza filamu kama walivyoahidiwa na waliopewa vyeti walipoenda kutafuta kazi waliambiwa kuwa ni feki.
Leo Soudy Brown amemtafuta Pastor Myamba na kumuelezea malalamiko hayo ambae amesema ni tetesi za muda mrefu, lakini kuhusu mitihani wanafunzi ambao walifanya mtihani walipata vyeti ila wale ambao walikataa hawakupewa vyeti, kuhusu ishu ya tamthilia amesema ni project wanayofanya wanafunzi wenyewe lakini wakati wa kushoot walikuwa hawaonekani.
Kuhusu vyeti kukataliwa wanapoenda kuomba kazi, amesema vyeti hivyo ni halali na vilitolewa na BASATA lakini baadae aligundua kuna mapungufu ambayo yaliwataka wawe wanafanya mitihani tofauti na awali, alipowaambia wafanye mitihani hawakuwa tayari na wao wanataka vyeti hawataki mitihani.
Bonyeza play hapa chini kusikiliza story yote…
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook