April 02, ni siku ya Usonji duniani yani watoto wanaozaliwa hadi kufikisha miaka miwili lakini wanashindwa kuongea, mtangazaji Emmanuel Likuda amesema ameamua kujitolea kuwa balozi wa watoto wenye matatizo ya usonji, ambapo atafanya mambo mbalimbali ili kuhamasisha na kupeleka uelewa kwa watu kuhusu tatizo hilo kutokana na uelewa kuwa mdogo ambapo atafanya tamasha Tar 30, April Escape One.
Jana kwenye 255, msanii Darasa alisema haoni faida yoyote ya kufanya biashara ya kuuza mziki online akiongea kwenye 255, digital Meneja wa Mkito Ismail, ambao wanafanya kazi na Darasa amesema ili msanii apate mafao lazima awe na data base mzuri ya Social Network , kwasababu kipato kinategemea watu wanaofungua link ya wimbo wake na msanii anatakiwa afanye jitihada za kujitangaza mwenyewe na kuwataja Fid Q na John Makini kuwahi kufanya vizuri kwenye mauzo.
Mchekeshaji Stan Bakora amekuwa akimuigiza mwanamziki Nay Wa Mitego jinsi anavyoongea, amesema kuna siku walienda kwenye show Nay akamtanguliza watu hawakujua kama sio Nay kutoka na kushindwa kuwatofautisha sauti zao na anapenda kumuigiza kwasababu ya kupenda kazi zake.
Bonyeza play hapa chini kusikiliza story zote…
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook