Wakati Arsenal na Manchester United wakizidi kusogelea katika kilele cha uongozi wa ligi kuu ya England, Chelsea leo imeikaribisha Stoke katika uwanja wa Stamford Bridge katika harakati za kujihakikishia nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa.
Mchezo huo uliomalizika muda mfupi uliopita, umeshuhudia vijana wa Jose Mourinho wakiongeza pengo la pointi dhidi ya wapinzani wao City, Arsenal na Man United baada ya kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Stoke.
Goli la Eden Hazard kupitia mkwaju wa penati katika dakika ya 39 liliwapa Chelsea uongozi wa dakika 5 kabla ya Charlie Adam kufunga goli zuri kutoka katikati ya uwanja na kuisawazishia Stoke City.
Kipindi cha pili Chelsea walipata pigo baada ya Diego Costa kudumu uwanjani kwa dakika 10 na kuumia, nafasi yake ilichukuliwa na Didier Drogba.
Loic Remy aliifungia Chelsea goli la pili na ushindi baada ya Hazard kufanya kazi kwa kupora mpira uliorushwa vibaya na golikipa Begovic.
Chelsea wamefikisha pointi 70 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi, Arsenal wanawafuatia wakiwa na pointi 64.
Kaa karibu na millardayo.com nitakachokipata nitakusogezea hapa muda wowote kuanzia sasa, unaweza kujiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook