Hakuna mtu yoyote ambaye ana ujasiri wa kutoogopa silaha, ndio maana ukikutana na story majambazi au wezi wameiba sehemu basi mara nyingi utakuta silaha zimetumika.
Tumesikia uhalifu mwingi sana ukitokea DAR na miji mingine mikubwa kwamba majambazi wanavamia sehemu wanaiba kwa kutumia bunduki.. nimekutana nayo mitandaoni kwamba Cape Town imetokea ya aina hii, taxi ilikuwa inatembea barabarani majambazi wakatokea na gari nyingine wakaizuia taxi kwa mbele.
Wakashuka jamaa wawili toka kwenye gari hiyo, wakawatishia bunduki watu waliokuwa kwenye taxi, wale watu wakashuka alafu majambazi wakamfunga kamba dereva wa taxi, wakamuweka kwenye buti wakaiba taxi na kuondoka nayo.
Polisi walifanikiwa kuwakamata baadae majambazi hao, lakini kilichonishtua ni kwamba hivi unaweza kuamini kwamba kile walichokionesha kama bunduki kumbe ilikuwa ni toy na sio bunduki ya ukweli!!
Japo hawakumdhuru mtu yoyote wakati wanaiba gari, silaha waliyotumia haikuwa bunduki ya ukweli.. Polisi wanawashikilia kwa sababu walichokifanya tayari ni uhalifu.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook