Taarifa zilizomfikia Soudy Brown ni ishu ya video queen ambao walikuwa wanafanya video ya msanii Matonya na Rich Mavoko kulalamika kwamba wamedhulumiwa fedha ya chakula.
Mmoja wa wasichana hao amesema baada ya kumaliza kufanya video walienda kula.. ilipoletwa bili ya chakula anasema Matonya aliwaambia wajilipie ila atawarudishia hela yao wakifika Hotelini.
Walipofika Hotelini hakuwapa hela yao, akawafanyia fujo na vitu vingine ambavyo wao hawakupenda.. wakamrekodi video akiwa anafanya hivyo…kambla ya kuondoka wakampigia simu Richie mavocal na kumweleza kuwa wameondoka na gari la Matonya, hadi watakapolipwa fedha zao, gafla walishangaa kumuona Matonya akianza kuwakimbiza, wamesema endapo Matonya hatawapa shilingi laki nane watavujisha video hizo.
Soudy alipomtafuta Matonya amesema walifanya video na ilienda vizuri, kuhusu wasichana hao kumdai amesema anajua kila kitu kilienda sawa ila kama wanamdai wampigie ili wamalizane.
Kusikliza story yote bonyeza play hapa chini mtu wangu…
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook