Maisha ya mtaani yana Hekaheka kila siku.. hii imesikika kwenye LEO TENA, inahusu mama ambae imesemekana kuwa hana maelewano na mtoto wake wa kike… wamegombana mara kwa mara kiasi kwamba hata majirani waliamua kuingilia kati.
Majirani wamesema kuwa mama huyo ana tabia ya kumtukana mtoto wake na kumnyima chakula, wakati mwingine anamfungia nje ya nyumba.
Mama huyo amesema mtoto wake hataki kumsikiliza, anafanya anavyotaka, akaamua kumfungia nje kwa sababu msichana huyo hataki kumsaidia kazi za nyumbani.
Msichana huyo amelalamika kwamba mama yake hamjali, akilalamika kwamba anaumwa hampi msaada wowote, wakati mwingine amekuwa akimsema kwamba ana ujauzito.. kuna wakati alitaka kwenda kukaa kwa bibi yake lakini mama yake alimkataza.
Bonyeza play hapa chini kusikiliza story yote…
millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook