Niliwahi kumuona msanii Kajala akitoa machozi kwenye Interview ya TV.. swali la kwanza kumuuliza ilikuwa ni lini mara yake ya mwisho amelia; “mi’ nalia kila siku.. sio kama napenda lakini ndio hivyo.. mtu akinikwaza kidogo au nikiwa nimeumia siwezi kuongea kwa hiyo kimbilio langu ni kilio..”
Wale wanaotembelea ukurasa wa Kajala wa Instagram watakuwa wameona, mara nyingi anapost picha za mtoto wake wa kike, Paula. Ana miaka 12 tu, unatamani kujua anamlinda vipi mtoto wake?; “Siruhusu hata mtu wangu wa karibu aniambie anamchukua Paula kwenda kula nae Ice Cream mimi nitampeleka nahakikisha niko around.. kama anataka kwenda beach lazima niwepo around namuangalia.. dunia ya sasa usimuamini mtu yoyote..“
Kumbe mpaka sasa hajamruhusu mtoto wake kuwa na simu; “Hana simu na hatokua na simu mpaka labda amalize form four..”
Kingine exclusive alichoshea na sisi ni movie yake mpya, kaa tayari kuikuta hiyo mtaani kwako mtu wangu, inaitwa PISHU, itatoka May 1 2015. Humo ndani kuna mastaa kama mchekeshaji Senga, Mzee Onyango na Hemedy.
millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook