Moja ya adhabu ambazo ziliwahi kumkuta mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli ni uongozi wa klabu yake kumpiga faini ya pound 25,000 pamoja na adhabu ya kukosa mchezo mmoja ambao walicheza na Arsenal kwa kuwatolea maneno makali mashabiki watatu ambao walimkashifu ishu ambayo ilihusishwa na ubaguzi wa rangi.
Mara nyingi Mario Ballotelli amekuwa akizungumziwa zaidi kwa upande mwingine.. ukorofi wake.. ishu za kutokuelewana na kocha wake na wachezaji wenzake.. wakati mwingine utasikia kazinguana na mashabiki.. huwa jamaa hachukulii poa kabisa ukimhusisha na story za ubaguzi wa rangi yake.
Utafiti umefanywa na kuonesha Balotelli ambaye kwa sasa ni mchezaji wa Klabu ya Liverpool ndiye mchezaji anayeongoza kwa kupokea post nyingi zaidi kwenye mitandao ya kijamii zinazohusu ubaguzi wa rangi katika msimu huu wa Ligi Kuu Uingereza.
Unaambiwa kwa msimu huu pekeake amepokea zaidi ya message 4000 huku kukiwa na nyingine zaidi ya laki moja za ubaguzi ambazo zimewalenga wachezaji ambao wana asili ya Afrika kwenye ligi kuu ya England.
Daniel Sturridge na Danny Welbeck pia wamefuatia kwa kupokea posts zaidi ya 1000 kila mmoja, zote zinahusu ubaguzi wa rangi.
Balotelli ni mmoja wa mastaa wa soka ambao wanatumia sana mitandao ya kijamii, labda hiyo nd’o sababu iliyofanya na wanaomshambulia pia kutumia njia hiyohiyo kumtumia post hizo.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter, instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook