Siku chache baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Togo na Tottenham Hotspurs, Emanuel Sheyii Adebayor kufichua siri kadhaa nzito za ugomvi na familia yake, mastaa kadhaa wa Afrika wamemuunga mkono kwenye hii ishu.
Moja kati ya mapacha wanaoiunda P Square, Peter amemuunga mkono Adebayor ambapo amemsifu kwa ujasiri wake na jinsi alivyojitokeza kuwa muwazi na kutoa yanayomsibu maishani mwake.
Peter ameandika ujumbe huu kumuunga mkono Adebayor >> ‘Ukweli ni kwamba hakuna mtu anayekudai lolote , familia yako inapaswa kuona fahari kuwa na mtoto kama wewe na si kinyume chake‘
Nyota wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Frimpong kwa upande wake aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter ambapo amesema kuwa baada ya kusoma kilichomsibu Adebayor anashukuru Mungu kwani familia yake ni kila kitu kwake.
Nyota wa Chelsea na mshambuliaji wa zamani wa Ivory Coast, Didier Drogba naye alionesha kumuunga mkono na amemuombea kwa Mungu na anajua ipo siku familia ya Adebayor itarudi katika msingi wa familia zote ambao ni upendo.
Didier Drogba ni mmoja kati ya watu ambao wamekuwa karibu na Adebayor katika kipindi hiki kigumu na inasemekana kuwa alizungumza na Adebayor saa chache kabla ya kuandika waraka mrefu kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Adebayor amefichua mgogoro mkubwa ulioko baina yake na ndugu zake pamoja na mama yake mzazi ambapo amesema kuwa kilichomfanya afanye hivyo ni kutoa fundisho na picha halisi ya jinsi ambavyo familia za Afrika zina shinikizo kwa vijana waliofanikiwa.
Dada wa Adebayor ambaye anaitwa Lucia amejibu waraka ulioandikwa na Adebayor ambapo amesema kuwa kila kilichoandikwa na staa huyu wa soka ni uongo na kwa sasa familia yake haimuhitaji.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.