Tumeishuhudia miaka nane ya mafanikio ya Bongo Star Search kuibua mastaa wa muziki Bongo.. Iliwahi kusikika Exclusive story kwenye #Amplifaya ambapo alisikika Madam Rita akiahidi kwamba msimu mwingine wa BSS unarudi on air!!
“Mwaka huu 2015 utakuwa ni msimu mzuri wa kusisimua.. Bongo Star Seach itakuwa kwenye Mikoa ya Arusha, Mbeya na Mwanza Pia itarushwa hewani kupitia Clouds TV na Star Tv kwa wakati mmoja pamoja na kuweka kwenye Youtube na mitandao ya kijamii“– Nimemnukuu Madam Rita.