Rapper Meek Mill aliziandika headlines siku chache zilizopita baada ya kuachia single yake mpya ya All Eyes on You aliomshirikisha girlfriend wake Nicki Minaj na Chris Brown.
Stori mpya leo ni kwamba Meek Mill amefanya interview kuzungumzia single yake na uhusiano wake na msanii Nicki Minaj. Kwenye interview hiyo Meek Mill alikuwa na haya ya kusema:
>>> “kuwa studio na Nicki sio issue kabisa, kwasababu yeye akiwepo mimi siwezi kuwa huru kufanya uchizi niliozoea kufanya nikiwa studio, yeye akiwepo aibu inakuwa kubwa mno, utakuaje serious kwenye kuingiza vocal kama demu wako amekaa hapo!”<<<
>>>“wimbo wa All Eyes On You ulikuwa ni wazo la Nicki, yeye ndiye aliyetengeneza ile single, alieyechagua beats na kunishauri namna ya kuingiza vocal zangu na zake, alikuwa tayari ana ramani ya kuifanya iwe radio hit. Mimi naimba navyojiskia tu.”<<<
>>> “Huu ni uhusiano wangu wa kwanza na mwanamke maarufu, mara ya kwanza mahusiano yangu ya kimapenzi kuwafuatiliwa na media, hiki kitu mimi kinaniboa sana,na mara nyingi nikiwa na Nicki namuomba tuwe tunaweka mambo yetu private”<<<
Kama bado hujaisikiliza single mpya ya Meek Mill, nimekusogezea hapa chini.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.