Deborah Oluwaseyi Joshua ni msanii kutoka Nigeria anayefahamika zaidi kwa jina la Seyi Shay. Seyi Shay ni mtunzi nyimbo, recording artist, performer na producer wa muziki aliyekulia Uingereza. Ameshwahi kuwandikia wasanii kadhaa nyimbo ikiwemo Wale, Chipmonk na Ne-yo.
Safari yake kimuziki ilianza kwenye kundi la muziki From Above lililokuwa lina simamiwa na Matthew Knowles baba wa RnB Superstaa Beyonce Knowles, akiwa chini ya kundi hilo walifanikiwa kusign mkataba na kampuni kubwa ya kurekodi, Sony/Columbia manger wao akiwa Matthew Knowles.
Kwenye interview moja aliofanya Seyi Shay alikaa na kuzungumzia changamoto pamoja na fursa alizozipata kupitia Industry ya muziki, Seyi Shay alikuwa na haya ya kusema:
>>>“Changamoto zipo nyingi, nimeshawahi kuimba mpaka nikahisi koo inanitoka lakini hakuna hata mtu mmoja alienipigia kelele wala makofi kwenye hiyo show, nimeshawahi kuanguka stejini na nikachekwa sana ila show ilibidi iendelee, sometimes nguo zangu stejini ziliachia na kunifanya nisimamishe performance hiyo kujiweka sawa.<<< Seyi Shay”.
>>>“Nilivyorudi Nigeria kutoka Uingereza nilipata changamoto nyingi haswa kuingia kufanya mziki Nigeria, ila kilichonisaidia nilikuwa tayari nimeshajengwa kuwa msanii so nilipopata team yangu nilioridhika nayo changamoto nyingi zilipungua”. Seyi Shay
>>> “Kwenye upande wa fursa, nimepata fursa nyingi kwenye industry ya muziki, kabla ya kuanza rasmi kuimba solo nilishawahi kuwa mmoja ya madansa wa Beyonce na chini yake tulitembea dunia na kufanya shows nyingi sana, alinifundisha mengi yaliyonijenga kama msanii, pia nimepata fursa ya kutembea dunia na kufanya shows nyingi”.
>>>“Nimeshawahi pia kumuandikia Wale nyimbo na kushare nae stage moja, nimeshare stage na Rick Ross, Wizkid, Fuse ODG na wengine. Pia nlishawahi kuwa kwenye kundi la muziki lililoitwa From Above wasichna 5 waliochaguliwa na baba yake Beyonce, alitupa training na kutumange kama kundi nae pia alinifundisha mengi kuhusu muziki na mpaka leo bado tunawasiliana”.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.