Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amekuwa kwenye headlines kwa wiki kadhaa sasa kutokana na kauli anazozitoa, Mourinho ambaye ni mtaalamu wa kucheza mechi nje ya uwanja kwa kuzivuruga timu pinzani kisaikolijia ameshaanza kauli zake.
Mourinho amekuwa na tabia ya kucheza na saikolojia ya timu au mchezaji hatari wa timu pinzani ili asiweze kucheza vizuri kwenye mechi, Mourinho ameanza kampeni zake za kumvuruga kocha wa Arsenal Arsene Wenger kwa kumsifia. Inaaminika kuwa Mourinho ameanza kumsifia Wenger ili aachane na umakini wa masuala ya usajili na kuanza kuamini kuwa kikosi chake ni bora msimu huu.
Kauli za Mourinho zinazoaminika zina lengo la kumtibua Arsene Wenger katika msimu huu wa usajili
“Chukua Calculator hivyo ni moja kati ya vitu rahisi kuvifanya, inaondoa uvumi wote kama unataka kuwa mkweli na ni kazi rahisi kwa kocha au muandishi wa habari kuifanya”>>>Mourinho
“Kama utajumlisha kiasi ambacho klabu ilitumia miaka mitatu au minne nyuma, nafikiri utakuwa unatafuta kushangazwa, wamemnunua golikipa mahiri na hiyo ni nafasi muhimu katika timu”>>>Mourinho
“kama utamjulisha Ozil, Sanchez, Chambers na Debuchy huenda ukapatwa na mshangao”>>>Mourinho
Kauli hii imetoka ikiwa ni siku chache toka kocha wa Arsenal akiri kuwa ilikuwa ngumu kwao kutwaa mataji lakini sasa wanaweza kutokana na usajili wanao hufanya lakini pia ni majibu kwa wale ambao hawaamini kwamba Wenger huwa hatumii fedha nyingi katika usajili…. Mourinho na Wenger watakutana mwezi August katika mchezo wa ngao ya jamii hivyo kauli hii inatafsirika kama njia ya kumdanganya mpinzani wako.
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.