Breaking news zilizoifikia millardayo.com saa nne usiku wa July 30 2015 kutoka Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) ni kwamba baraza hili limemfungia Shilole kutojihusisha na kazi yoyote ya sanaa kwa muda wa mwaka mmoja.
Barua iliyoifikia millardayo.com ambayo imeandikwa kutoka BASATA imesema >>> ‘Tarehe 9 May 2015 ukiwa katika onyesho lako la muziki Ubelgiji ulicheza uchi mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za Tanzania hivyo kudhalilisha utu wako na jamii ya kitanzania kimaadili‘
‘BASATA ilipata habari zako, kumbuka pia October 2013 BASATA lilikuonya na ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza bila kuzingatia maadili uwapo jukwaani, BASATA ilikupa nafasi ya kutoa maelezo kwanini usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chako lakini umekaidi kutoa maelezo yako‘ – BASATA
‘Baraza limejiridhisha kwamba ulikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye onyesho lako huko Ubelgiji makusudi na umekiuka sheria kwenye ibara ya 30 (2) ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuvunja maadili ya jamii ya Mtanzania hivyo baraza linakusimamisha kujishughulisha na kazi za sanaa nchini na nje ya nchi kwa mwaka mmoja, kufanya kinyume na hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi pamoja na yeyote utakaeshirikiana nae ‘ – BASATA
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.