Shirikisho la Soka ulimwenguni FIFA huwa na utaratibu wa kutangaza viwango vya soka vya nchi wanachama kila mwezi lakini Tanzania imeonekana kuzidi kushuka, ndani ya kipindi cha miezi miwili imeshuka kwa nafasi 13 hii inatokana na matokeo mabovu kwa mechi za Taifa Stars za hivi karibuni.
Tanzania mwezi uliopita iliporomoka hadi nafasi ya 139 na mwezi huu imeshuka tena hadi nafasi ya 140 ikiwa imeshuka kwa nafasi moja tena. Licha ya TFF kumfukuza kocha Mart Nooj kufuatia mwenendo wa matokeo mabovu na nafasi yake kuchukuliwa na kocha Charles Mkwasa lakini bado haijawa suluhu ya Stars kupata matokeo mazuri.
Stars imekuwa na matokeo mabovu kwa mechi za hivi karibuni kwani ilifungwa mechi zake zote tatu za kundi B katika michuano ya COSAFA ambapo Tanzania ilishiriki kama timu mwalikwa, mechi ya kwanza kufuzu AFCON ilifungwa goli 3-0 na Misri baada ya hapo ikatolewa na Uganda kufuzu michuano ya CHAN 2016 kwa jumla ya goli 4-1.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos