Producer mkali Bongo, Nahreel kumbe yupo kwenye mpango wa kufungua chuo cha Production ya muziki?? amesema mafunzo ya production yataanza hivi karibuni na yatachukua wanafunzi wengi ambao wanahitaji kujifunza mambo hayo.
Nahreel amesema kwa yeyote atakayehitaji kujiunga taarifa zitawekwa kwenye mitandao ya kijamii, sifa za mtu anayetaka kujiunga kwanza ni kuwa na idea ya muziki ama awe anapenda muziki.
Kingine amesema mpango ana mpango wa kuanza na wanafunzi 30 na kuendela na ada itakua si kubwa ili kila mtu ambaye atapenda kujiunga ajiunge na masomo hayo… hii ni good news mtu wangu !!
Juru sio jina geni Bongo Flevani, jamaa aliwahi kutoa hit ya wimbo wa ‘Mburura’ alafu ikawa kama amekaa kimya kwa muda mrefu hivi… kumbe kimya chake kina sababu, moja kubwa ni ishu ya baba yake mzazi kufariki… Pole kwa mtu wetu, baba wa Juru kumbe alikuwa anatoa support kubwa sana kwenye muziki anaofanya jamaa.
Sababu nyingine ya ukimya wake kumbe ni kutokana na ishu ya Management, uongozi wake haukua mzuri ndio maana baadhi ya nyimbo zake zilikua hazifanyi vizuri.
Yuko Rapper mkali toka Kenya, anaitwa Rabbit ambapo ana story kuhusu kiasi cha pesa ambacho kama unahitaji kurekodi ngoma au video yako Kenya unatakiwa kukitoa.
Rabbit amesema kwa studio ya ukitaka kurekodi audio unatakiwa kutoa kama laki 3 ya Tanzania hadi milioni 1, ila kwa upande wa Video ni kuanzia milioni 2 na kuendelea ambayo inajumuisha kila kitu mpaka mzigo unakamilika.
255 na stori zote iko hapa mtu wangu, unaipata yote ukibonyeza play.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos