Baada ya kuachana na mchumba wake miaka miwili iliyopita mwimbaji wa R&B Christina Milian alianza kuonekana sana na rapper Lil Wayne baada ya kujiunga na lebo ya msanii huyo, muda mfupi badaae wawili hao wakaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na mpaka sasa wana zaidi ya mwaka mmoja pamoja.
Lakini leo headlines za wawili hawa ni tofauti kidogo… wapenzi hao wamethibitisha kuwa wameachana toka mwezi uliopita lakni waliamua kukaa kimya kwanza na kuweka baadhi ya mambo yao sawa kabla ya kutangaza kwa watu kuwa uhusiano wao wa kimapenzi umeisha.
Msemaji wa karibu wa watu hao anasema sababu kubwa iliyopelekea kuachana kwao zinatokana na ratiba za wawili hao kubana sana.
>>>“Wanaachana sio kwamba wanapenda ila ratiba zao zinawabana sana, wanakosa muda wa kuonana na kuwa pamoja, Lil Wayne anafanya sana tour za wasanii wake na za kwake pia na pia anaifanyia kazi album ya Christina Milian… isitoshe hata Christina Milian ana mambo mengi, vipindi vya TV, Talk Shows za kuandaa na vingine vingi, so wameona bora waachane lakini sio kwa sababu wamechokana ila ratiba za kazi haziwapi muda wa kutosha kuwa pamoja”. <<< Alisema msemaji wa karibu wa mastaa hao.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos