Kwa mtu ambae anafatilia sana movie majina ya mastaa kama Angelina Jolie, Will Smith au Bruce Willis sio mageni kwao… hao wote ni mastaa wanaofanya poa wakiiwakilisha industry ya Hollywood Marekani.
Nimepata kitu kingine kilichonivutia mtu wangu, unajua ni rahisi kumuona mtoto wa staa wa movie kwenye Movie za Bongo, tena urahisi wenyewe ni kwamba staa mwenyewe anaweza kumshika mkono mwanae akaenda nae location na mtoto nae akawa na scene yake ya kucheza.
Marekani mambo sio rahisi kiasi hicho, unaambiwa kama una mkataba na Will Smith basi ni wewe na Mr. Smith mwenyewe, masuala ya kumuingiza mtoto wake kwenye movie hiyo ni biashara nyingine kabisa.. yani mtoto nae lazima awe na mkataba wenye malipo yake kabisa, baada ya kukamilika kila kitu mambo mengine yanaendelea.
Kuna movie nyingi kumbe mastaa wako na watoto wao aisee, utaratibu ni huohuo wa Mikataba… nimeipata stori ya baadhi ya mastaa ambao wamewahi kucheza Movie pamoja na watoto wao Marekani mtu wa nguvu.
Kuna movie yoyote kati ya hizo umeiona mtu wangu? Ipi umeipenda zaidi ukaona mzazi na mtoto wake walivyotisha ndani ya Movie?
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE