Chris Brown na lile jinamizi la kesi Mahakamani bado havijamwacha salama… ana tour ambayo anatakiwa akafanye Australia mwezi December 2015, story zimefika mitandaoni na kwa tetesi zinazoongelewa mpaka sasahivi ni kwamba huenda hata asiruhusiwe kukanyaga ndani ya nchi hiyo.
Serikali imetoa Taarifa kwamba wanayapitia upya maombi ya viza ambayo Chris alifanya kwa ajili ya kufanya tour hiyo… bado wanakumbuka kuhusu Kesi yake ya kumpiga Rihanna japo Mahakamani mambo tayari yaliisha.
‘Watu wanatakiwa wajue kwamba kama una makosa ya jinai na unahitaji usafiri maeneo mengine Duniani, kuna nchi ambazo hawahitaji watu wa aina hiyo watembelee nchi zao’- hiyo ni nukuu ya alichokisema Waziri wa Masuala ya Wanawake Australia, Senator Michaelia Cash.
Chris sio wa kwanza kuzuiwa kuingia Australia, February 2015 Bondia Floyd Mayweather alizuiwa pia kuingia Australia kwa sababu ya ishu ya kuwa na Rekodi ya Makosa ya Jinai ikiwemo kuwafanyia ukatili wanawake.
Hiyo ni post ambayo jamaa mmoja kaiweka kwenye ukurasa wake wa Twitter, kuna hiyo picha ya tangazo ambalo linaonekana limebandikwa kutangaza ujio wa Chris Brown Australia, alafu akaja mtu mwingine akaandika >>> ‘I BEAT WOMEN (NINAPIGA WANAWAKE)‘>>> Jamaa aliyepost pia picha hiyo anaonekana kusupport ishu ya kumzuia Chris asitue nchini kwao !!
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE