Siku chache baada ya Taasisi ya TWAWEZA kutoa Ripoti ya Utafiti waliofanya kuelekea Uchaguzi Mkuu Tanzania, October 25 2015… Viongozi wa Vyama mbalimbali wametoa misimamo yao kuhusu Utafiti huo.
Jana September 23 2015 January Makamba alitoa Taarifa kuhusu msimamo wa CCM kwenye Utafiti huo, ninakusogezea na hii pia mtu wangu, Taarifa kutoka Makao Makuu ya ACT- Wazalendo Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni wa Chama cha ACT-Wazalendo, Nickson Tugala alitoa taarifa hiyo >>> “Chama cha ACT kimeyapokea na kuyapitia Matokeo ya utafiti uliofanywa na TWAWEZA… Utafiti unaonesha Ilani ya ACT imezingatia mahitaji ya Watanzania“>>>
“ACT tunafarijika kwamba Chama chetu ni Chama pekee nje ya CCM na UKAWA kilichotajwa na Wapigakura zaidi ya Asilimia moja, kimekuwa chama cha nne katika kukubalika kwa Wapigakura nyuma ya CCM CHADEMA na CUF” >>> Nickson Tugala.
“Takwimu hizo zilikusanywa wakati ambao ACT-Wazalendo hakijamtangaza Mgombea wake wa Urais wala tulikuwa hatujafanya Uzinduzi wa Kampeni… Kama Utafiti huu ukirudiwa tunaamini tutafanya vizuri zaidi” >>> Nickson Tugala.
Sauti yenye Taarifa yote hii hapa mtu wangu, Ripoti kutoka Makao Makuu ya ACT- Wazalendo Dar es Salaam.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE